Saturday, January 14, 2017

SURA YA 6



SURA YA 6
Baada ya muda wa dakika thelathini hivi Pendo alimletea Rashid maziwa ya pakiti na biskuti za Manji.
“Bwana we chukua hizi zako ili utoe woga wa mahojiano…” Pendo alimtania Rashid huku akimshika kiganjani kwa mkono wa kushoto.
Rashid alitabasamu huku wakitembea hadi uga wa chuo.
Kulikuwa na vivuli pale kando kando ya uwanja wa chuo.
Waliketi kwa pamoja huku Rashid akitoa ushuhuda wa mahojiano asubuhi ile akipata funda la maziwa na kitafunio.
“Pendo unaamini nitapata nafasi ya ajira kweli?
“Ndiyo sababu najua wale majaji vizuri na mie ndiye nalikuarifu kuhusu mahojiano ya leo na  kazi ushapata…”
“Acha utani mrembo wee…”
“Mie sipendi mchezo kwa kazi na ndiyo maana nakwambia utapata nafasi ya kujenga taifa letu.”
Rashid aliangua kicheko hadi maziwa yakamsakama ikambidi Pendo aanze kumfanyia huduma ya kwanza pale uwanjani.
***
Baraza alitoka kazi siku ile ya Jumatano mapema sana. Ilikuwa mwendo wa saa sita mchana.
Alikuwa anatokea kwa zahanati ya kaunti pale mjini.
Alienda huko kwa sababu hamna adaa zozote zinazotozwa kwa mwananchi wa kawaida. Hii ni kulingana na sheria ya rais ya kumfkia mwananchi wa kawaida.
Vile vile wakati wa kupiga kura ulikuwa umekaribia sana. Kwa hiyo mwananchi alipewa na kupata chochote kutoka kwa viongozi hawa na watarajiwa pia kipindi hiki.
Baraza alijilaza kitandani kutokana na kulemewa na zile tembe alizopewa na dakatari za nne mara nne kwa siku.
Pale kitandani alikuwa anakoroma mithili ya gari zee la mzee Bakari pale vijijini. Lile gari lilikuwa linatoa moshi na sauti ya kuwafanya waliolala kuamka na kupiga chafya bila kisuizi.
Aliota ndoto saa tisa mchana.Aliona nduguye Rashid ameoa mke mrembo.
Mke huyo alimfanya Rashid kuonekana nadhifu kushinda alivyokuwa mpweke.
Rashid alizungumza kwa lugha ya kizungu tupu.
Alipokuwa akizungumza ungedhani alizaliwa ulaya na kujipata barani Afrika kwa bahati mbaya. Aliwazungumzia hata wazazi wake ambao walikuwa mbumbumbu lugha hiyo ya mstuko wa moyo kwao.
Siku zote Rashid akukosa chakula wala mavazi ya kisasa.
Vyote alivyokula na kuvalia vilitoka katika maduka ya kijumla ya walala nacho.
Katika biashara,yeye ndiye alikuwa mwenyekiti katika Afrika mashariki. Allimiliki kampuni za tarakilishi, magari,maji,mazao ya kilimo, vinywaji kali na vitamu na mahoteli ya kifahari bila kusahau skuli za kutajika nchini kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.
Popote alipokaa au kunywa chochote,lazima kulikuwa na na bidhaa ya kampuni yake.
Mkewe pia alikuwa na sura ya kudondokwa na ute kwa waume na kuonewa gere na wake waliomuona.Mbali na urembo yeye alikuwa mchapa kazi. Alikuwa siku zote mkali sana kwa alilosema na kutenda na mgumu wa kucheka ovyo. Naye alikuwa anamiliki maduka ya jumla nchini ya mavazi ya kike na vipodozi. Alikuwa mwanabiashara shupavu na pia mpiganiaji haki za wanawake barani Afrika.
Wakati mmoja alipewa tuzo ya Nobel kama mama mkarimu na mpenda watoto wa bara Afrika. Alikuwa amezindua vituo kadhaa barani vya kuwanusuru wanasichana kutoka kwa ndoa za mapema na kupaswa tohara.
Mkewe Rashid ndiye mwanamke wa kwanza kuwapa wanafunzi wa kike vipatakilishi katika masomo yao ya msingi kwa walemavu na kujenga sehemu ya kuwajali wakongwe.
Baraza yeye alikuwa dereva tu wa nduguye. Wakati mwingine nduye alimpiga kwa maneno makali bila kujali kuwa yeye ni wa toka nitoke.
“Aise hatumii akili au ndiyo maana ulifeli skuli.”
“Iweje mie mdogo wako nina hela nawe ni kuniomba tu huku,nahitaji kuwekeza bwana kwa vitu za faida bwana,tafuta jasho lako.” Maneno haya yalikuwa wimbo kwake Baraza lakini ilimbidi kumeza tu kama maji ya kukata kiu.
Siku moja mkeo Rashid alimnyangaya ufunguo wa Mercedez Benzi ya E-Class. Alimwambia kuwa ana ufundo wa jana kutwa kwa hiyo hangempa bahati mbaya ya siku. Alimfukuza hadi nje ya kasri lile lilokuwa katika shamba ya garden estate pale jijini katika hekari kumi. Alimpa amri mlinzi kuwa shemejiye asionekane pale.
Rashid licha ya kuwa bwenyenye wa kumezewa mate pale mjini,hakufanikiwa kumpata mtoto. Alitumia mbinu zote za waganga wa kisasa na wa zama,lakini yote bure bilashi.
Baraza njiani alikuwa anajiuliza mengi baada ya shemeji kumtema asubuhi ile ya saa mbili na nusu. Kulikuwa na manyunyu alipotemwa bukrata ile.
“Mola mbona mimi?Mbona niwe omba omba? Mbona mdogo wangu kufanikiwa huku mjini na mimi ndimi nilimleta,Mola mbonaaaaaaa…..
Ghafla aliamka kwa kumaka yale maneno ya ndotoni mbona kwa sauti iliyowafanya wapangaji kuweka umati pale mlangoni.
***


Wosia wa mama
Mwanangu skiza,wewe ‘angu wingu,
Kwangu wakaza,ewe anag’za wangu,
Zangu ahadiza,wewe z’disha ‘wangu,
Nakala nakupa,wakala ‘angu wewe.

Siku zangu kwisha,wewe hutakwisha,
Moyo wangu s’fisha,k’bla s’jakwisha,
Skiza yangu kwisha,muda s’jakwisha,
Maneno haya,mwanangu yawekee.

Roho inadunda,wewe gwiji ume,
Cheti niliunda,m’mliki wewe ume,
Chuo niliunda,akili yako ume,
Njia niliunda,ona mbele wangu.



Pendo alikuwa akikariri shairi ili kwake Rashid mchana ule kabla ya kupata ujumbe kwenye simu yake.
’Hebu mweleze Rashid aje andikishe kandarasi yake saa nane.’
Huyu alikuwa Prof vile Pendo alikuwa amemnakili katika simu yake.
***


SURA YA 7
Rashid waliwasiliana na Pendo tangu usiku ule alipomsaidia. Walikutana pale Tom Mboya baada ya miaka miwili ya mawasiliano ya simu tamba.
“Nashukuru Mungu kukuona mchana wa leo.”
“Nami pia ingawaje umebadilika sana,naona misuli huku,unazungumza lugha ya sheng kabisa…
“Acha mzaha bwana,usisahau kuwa ulinisaidia kushinda neno lenyewe,kusaidia.”
“Karibu bwana,hiyo ilikuwa kidogo tu.”
Hapa walikuwa wakipiga gumzo katika mkahawa wa Hilton Hotel.Kwa umbali na mazungumzo yao ungedhani kuwa wameonana kwa muda na ni kama mtu na nduguye.
“Waona huyu kuku tunaye mla yuko sawa na  kabisa na Yule niliporwa pale Country Bus ile ayami nilikuja mjini,ule usiku ulinisaidia. Tafauti ni kuwa huyu amepikwa na wangu alikuwa hai. Walipiga kichekeko mle ndani hadi wateja waliokuwemo wakwatazama kama sinema.
“Rashid tosha tafadhali naomba tuwe na nidhamu ya mezani.”
“Sawa,nimetii amri.”
Baada ya sekunde chache Rashid aliuza,”Pendo mbona karibu mikahawa yote hapa mjini ukiitisha chai wanakupa karibu kila kitu kando kando baadala ya wao kupika kwa pamoja;sukari,maziwa moto,machani,kijiko…
Walianza tena kucheka. Ilikuwa mwendo wa saa kumi na moja walipotoka mle ndani.
Hapo ndipo Pendo alimweleza Rashid kuwa yeye ni mwanafunzi katika chuo kikuu na taaluma yake pale chuoni. Vile vile yeye ni mwanamtindo na mwanabiashara asiyejulikana.
Hapo kwa biashara ndipo Rashid hakuelewa ni vipi mtu mhudumu asijulikane hata na mteja wake.
“Naamanisha kuwa mimi nina biashara huku mjini,hasa za mavazi ya kimitindo na kazi hii nimeandikishakwa rafiki zangu sio mimi.”
“Mbona ukamua kufanya hivo baadala ya wewe mwenyewe kujiandisha.”
“Hamna tafauti Rashid kuweka jina la bui yako au mimi. Kumbuka utamu wa biashara ni pesa na wao uniwekea hela hizo kwa benki kila siku.”
“Utajuaje kuwa kuna yule ambaye hajaweka pesa kwa akaunti yako sasa ukiwa skuli?”
“Mimi utumia njia ya simu tu sababu kifaa hiki kina uwezo hata wa kunionyesha matukio ya biashara kwa picha na maandishi kama sasa angalia…
Rashid aliona ukurasa mpya wa maisha kwa aliyo yaona na kuskia kutoka kwake Pendo.
Kweli jina na tabia lilimfaa yeye, Pendo.
“Yaani una uwezo wa kujua mali yako kupitia hiki kifaa tu?”
“Mmh!” Pendo alitikiza kichwa.
“Kweli umenizingua wewe ni moto usiochoma.”
Uhusiano wa hawa wawili ulipanda ngazi kwa kasi bila yeyote kutumia nguvu za kimabavu.
***
Pendo alipomaliza kusoma ule ujumbe mfupi,alimshawishi Rashid waende kutali chuo chao.
Walikuwa wakipiga gumzo njiani huku Rashid akijiuliza mengi akilini na moyoni.
“Je nitapata kazi hii?”
“Nikipata kazi hii nitalipwa pesa ngapi?”
“Je, Pendo anaweza kuwa nyota yangu ya jaha katika hali yangu hii ngumu?
Pendo alikatiza fikra za Rashid, “Bwana wee hebu ingia mle ofisini,mlango wa kwanza huo kulia, mna ripoti yako hapo,nakusubiri hapa nje.”
Rashid alishtuka kama kwamba si yeye aliamrishwa na Pendo.
“Mimi au nani?”
“Ah,ni Rashid.” Pendo alimjibu.
Baada ya Rashid kujizoazoa alibisha mlango.
“ko ko ko”
“Karibu ndani. Nikusaidiaje?”
“Asante kwa kunikaribisha humu ofisini. Mimi naitwa Rashid na nilikuwa mmoja wa wahojiwa humu asubuhi…”
Ok Rashid nimekuelewa. Kwanza ongera kwa kufaulu katika mahojiano ya leo. Subiri kidogo mtaonana na Prof ili ujaze fomu zako za kazi.”
Yule binti aliyemkaribisha Rashid alichukua simu akampigia Prof.
Hello sir,Rashid amefika.”
“Mruhusu aingie ofisini kwangu.”
“Asante prof.”
Rashid alijaza fomu mingi hapo ambazo katu maishani mwake fomu hizo hajawahi jaza hivo mbali na zile za kutahiniwa alipokuwa shule ya sekondari.
Aliitishwa nakala za cheti cha kutoka kwa polisi,kadi ya malipo ya uzeeni,kadi ya hospitali ,kitambulisho,picha tatu za passport,akaunti ya benki,kadi ya kulipa ushuru na ripoti kutoka kwa daktari ya hivi punde kuhu afya yake.
Alipomaliza kujaza na kuweka sahihi alipewa sare zake za kazi na kuarifiwa kuwa kuna gari linalobeba wafanyi kazi kila siku kuenda na kurudi nyumbani. Aliambiwa amepewa juma moja kufanya matayarisho ya kuanza kazi.
Alichukua saa moja mle ndani alipokutana na Pendo. Alimshukuru sana na kumpiga busu mbele ya ofisi alipopewa barua ya kazi katika chuo hicho.
***
Baraza aliposhtuka kutoka usingizini,alishangaa kuona watu mlangoni kwake.
Alipotaka kujua kilichowaleta kwako,alipigwa na butwa aliloambiwa.
“Bwana si tumefikiri kuwa una kiruka njia hapo ndani anayekuadhibu.”
“ sisi kukusaidia na unatuliza tunafanya nini hapa? Mmoja wao alimuuliza.
“Bwana mdogo,una kichaa vipi?” bibi mmoja mnene na ngozi ya makaa alimuuliza.
Baraza alipoona maswali yamememzidi  aliweka komeo na kutoka nje akielelekea katika uwanja wa watoto pale mtaani.
Alitafakari sana kuhusu ile ndoto sababu bado ilikuwa akilini mwake.
Aliwatazama watoto wakiwa wanacheza mpira wa mguu lakini mawazo bado yako ndotoni.
Ilikuwa mwendo wa saa moja jioni alipotoka pale uwanjani. Alimpigia nduguye simu na kumuuarifu aje na madodo na chapati nane.
***
Masinde Muliro Gardens pale Kakamega saa nne asubuhi Jumamosi ndiyo siku maalum kwa hawa wawili;Pendo na Rashid.
Rashid huku alikuwa mwenyeji naye Pendo alikuja kutalii na kujionea mazuri ya pande za magharibi mwa Kenya .
Hii ilikuwa shukrani ya pekee kwa Rashid kwake Pendo kwa lile fanikio lake la kazi.
Alimhadi kuwa mshahara wake wa kwanza angempeleka Pendo Maghari kujionea mandhari safi ya kufurahisha macho na kutoshelesha mwili.
Na hakika hilo alitimiza Jumamosi hiyo.
Alimpeleka Pendo kuona ule mchezo wa fahari wawili wanaopigana huku umati ukishangilia kwa alaa za muski wa kitamaduni.
Pia walielekea mlima Elgon na kutembelea mbuga ya wanyama pori. Walifanikiwa kuwaona simba marara,fisi,konokono,njiwa na wanyama wengine waliokuwa na majina ya kitamaduni. Picha walipiga sana,hasa zile za selfie.
Lilomfurahisha Pendo hadi sasa ni vile familia nyingi pale magharibi wanavyopenda kumbikumbi kama kitoweo.
“ Awa ni watamu sana zaidi ya nyama wa mjini,”Rashidi alimweleza Pendo.
Siku ya jumapili nayo Rashid aliandamana na Pendo hadi ukumbi mmoja. Mle ndani jogoo walikuwa pia wanapigana. Ndege hao walikuwa wakubwa mfano wa mwana kondoo kwa umbo.
“koo koooo” ndiyo ilikuwa sauti ya kuwapa motishia wale jogoo.
Siku yao ilikamilika wakiwa katika uga wa Webuye Pan Paper. Pale kulikuwa na mashindano ya uwendeshaji baiskeli kwa kina mama hamsini waliojitokeza.
Mama mmoja mwenye umri wa miaka sabini aliwabiku mabinti wote na kutunukiwa taji Piki piki na hundi ya elfu hamsini baada ya mchezo huo.
Jioni hiyo walifika mjini Eldoret na kuabiri ndege hadi mjini Nairobi.
Kila mmoja alikuwa ametulia sababu ya uchovu wa siku mbili. Hata Rashid msema mengi hakuwa na usemi siku hiyo.
***
Asubuhi ile ya jumatatu Rashid alikuwa katika kituo cha matatu kungoja basi la kusafirisha wafanya kazi wa chuo.
Alionekana nadhifu ndani ya zile sare za rangi ya bluu. Sare zile zilikuwa na nembo ya mwajiri wake. Viatu vyeusi tititi vilitii amri ya mngaro wa rangi ya kiwi.
Wajihi wake ulijawa na tabasamu. Aliamkua wafanya kazi wenza waliokwemo. Aliripoti kazi yake pale langoni. Kwa mujibu wa mwajiri wake yeye mwenyewe alikuwa na kitambulisho cha kazi kilicho ninginia pale shingoni na alipashwa kukagua yeyote anaingia chuo. Aliandikisha kila mgeni kwa daftari alilopewa kwa majina,saa,anakoenda na nambari ya kitambulisho chake au paspoti. Mgeni alipotoka alifaa kutia sahihi kabla ya kurejesha kadi ya mgeni.
Saa nne asubuhi aliletewa chai kwa mkate uliopakwa mafuta.
Rashid pia alikuwa akipata Baraka ya chakula kila mchana kutoka kwake Pendo.
Jioni ya saa kumi alifaa kumaliza zamu yake na kumkabidhi mwenziwe ripoti ya siku.
Kabla ya kuchukua lile basi lilomleta,ilikuwa mazoea lazima amuone Pendo ampe kwaheri.
Kila wikendi angekuwa naye Pendo anayemchanua kila kunapokucha kuhusu mbinu za kuhishi mjini.
Ni miaka mitatu sasa tangu Rashid kuajiriwa pale chuoni kama mlinzi. Ameweza kufungua maduka mawili pale Kiambiu na nduguye ndiye anasimamia huku akipata ripoti kila wiki.
Mashambani pia alikuwa amenunua tarakilishi hamsini zinazotoa huduma za uchapishaji wa nakala mbali mbali. Pale pia babake ndiye anayesimamia na mamake anasimamia ngo’mbe,mbuzi kondoo,kuku na ndege wa quil.
Mbinu zote za mafanikio haya alipata kutoka kwa Pendo anayesomea uzamivu wa usimamizi wa biashara katika chuo hicho.
Rashid alikuwa amepandishwa cheo kazini hadi kuwa nyapara. Marupurupu yalikuwa sawa kwake sababu hakukosa lishe ya siku.
***


SURA YA 8
Baraza alipomwarifu nduguye kuja na chajio, alienda kwa bafu kukoga sababu alijihisi ni mnyonge sana. Ni siku ya nne sasa tangu yeye kunawa mwili.
Alifanya vile sababu kwake maji yalikuwa bei ghali. Mtungi mmoja wa lita ishirini ulikuwa shilingi tano,bei ya andazi kwa chai.
Bado akikoga ile ndoto alitafakari sana sababu hajawahi kuwa na njonzi kama hiyo.
Alichukua nusu saa kuoga na alipomaliza alimpata nduguye akiskiza redio.
Kilikuwa ni kipindi cha kusoma kadi za salamu.
“Hapa kadi ya salamu ni Wanyama kutoka Shemakho,anawasalimu,Joseph Wanyama,Truphena Wanyama,Musa Wanyama,Junia Wanyama na ujumbe ni kuwa wasiwe wachoyo msimu huu wa krismasi…”
“habari ya siku kaka?” Baraza alimsalimu nduguye huku akijipaka mafuta mwilini.
“Safi hofu kwako.”
“Kabisa hofu yangu ni kuwa mwili leo umeninyima raha.”
“Wamaanishaje mkubwa wangu?”
“Leo nimekuwa hospitalini,daktari ameniambia kuwa nina niumonya.”
“pole nudge. Ugua pole lakini mbona unakoga maji baridi tena?”
“bwana wee vipi ulitaka nitumie makaa kuchemsha maji na makaa bei ghali?”
Mazungumzo yale yalendelea kwa muda kabla ya Rashid kupasua mbarika ya kazi yake mpya katika chuo kikuu,pale mjini.
Alimpa hadithi vile alivyopata nafasi hiyo na kuwashinda watahaniwa hamsa.
“aliyefanya nipate hiyo kazi wajua ni nani?” Rashi aliuliza nduguye.
“Sijui hata.”
“ni Yule banati aliyenisaidia ile siku nilikuja mjini siku ya kwanza.”
“Yule anaitwa Penn…Peninnah…Periz…haa mbona nasahau hivi…”
“Ni Pendo bwana. Unasahau haraka aje nawe.”
“Hongera bwana ila wafaa kujiadhari kabla ya ha….”
Rashid alimkatiza usemi nduguye.
“vipi nawe. Kwani kuna hatari ipi ya kupata ajira kihalali? Mie nataka ajira ili nipate jasho langu na kuwekeza.”
“sawa sawa ila usije ukalia baadaye. Kumbuka shamba la mjini ni mwamba kwa mkulima wa kijijini.” Baraza alimpa nduguye hiyo nasaha.
Lilomkera sana Baraza ni matukio yake na Pendo baada ya mahojiano. Alitafakari ni mwanamke wa jinsi gani anampa mwanaume maziwa,biskuti, kazi,mazungumzo…akajijasia mengine kuwa hata labda naye Pendo amempa kandarasi ya kumkanda!
Rashid alimuonyesha barua yake ya kazi na mshahara wake ukiambatana na marurupu yake.
Pia alikuwa na begi jipya la Nike la mgongoni lilokuwa limebeba viatu,nguo, kofia, kitambulisho cha kazi na nakala ya jarida la chuo hicho.
“ Sasa umepangaji na mshahari wako wa kwanza? Baraza alinena
“ Haah!  Bwana una mbio aje. Kuwa mpole hata sare zenyewe sijifaa nione zinavio nIkaa mwilini.”
“Si kwa ubaya sababu nitahitaji ulipe kodi ya mwezi huu na unipe mkopo wa elfu kumi…”
“ Tosha bwana kwani una kichaa, unapangia vitu  ambavyo hata kibeti change hakijaskia harufu yake wala kuona sura. Aise heshima idumu. Sawa?
***
Baada ya busu la muda baada ya kupewa barua yake ya ajira,Pendo alimpeleka Rashid hadi Kampus Mall kwa,kando ya chuo hicho kwa kikombe cha chai.
“Rashid hongera kwa kupata ajira.”
“Asante pia kwa wema na fadhili zako kwangu.”
“mie napenda mtu wa kuchapa kazi. Mwenye bidii ya mchwa. Anayeona zaidi ya pua lake. Aliye na uwezo wa kutabiri kesho yake. Mtu huyo ni wewe Rashid. Usinifeli nakuomba.”
Kimya kilitanda pale kwa sekunde.
Rashid alimtazama Pendo kwa macho ya usikivu.
Alishikilia kikombe kile kwa muda mrefu kabla ya kufungua kinywa chake.
“Pendo nimekuskiza kwa makini. Nimekuelewa Pendo. Hitaji lako Pendo, timizo langu nakuahidi Pendo. Siwezi na sina nia ya kukufeli mimi Rashid.”
Rashid aliendelea,”iweje nimewashinda ule umati katika kazi hii yangu mpya?”
“usijali Rashid,Yule Prof ni mwendani wangu wa karibu sana. Stori ya uhusiano wangu naye ni refu lakini nitakupa mukhutasari.
“siku moja Prof alikuwa mgonjwa. Alikuwa si hayati si mamati. Alikuwa na shida ya figo. Hapakwa na mtu wa kumpa nafasi ya kuhishi tena kutoka kwa aila yake kwa kumpa figo.