Wednesday, September 21, 2016

SURA YA TANO
Usiku ule Pendo alipomkuta Rashid alikuwa ametoka masomo yake ya nyanjani pale Gizani skuli.
Alikuwa akibarizi mji mkuu. Kupata hewa ya wajanja. Alikuwa akitoka kupata chajio pale Afya Centre.
Pia alipitia Ken Chic kununua kaukau .alipenda sana kutavuna kaukau alipokuwa mjini.
“ah!sijapitia Taveta Court kuona mavazi mapya.” Alijiambia.
Alielekea pale kuona mavazi hasa ya kujikinga na baridi. Ulikuwa mwezi wa agosti. Huu mwezi kuna baridi na umade sana mjini. Alijipima koti lilojulikana kama trench coat.
Katika harakati za kurudi bwenini kabla ya mlinzi kufunga ndipo alipokutana naye Rashid.
Alimwonea huruma. Hajawai kuwa na moyo wa msamaria mwema kwa mtu yeyote hivo isipokuwa huyu kijana.
Alihisi moyoni kuwa amtendee wema adinasi huyu.
Alipomdadisi moyoni alimwona huyu katu si mjanja wa mjini.
***
Siku ile Pendo alimaliza masomo yake ya nyanjani pale skuli ya Gizani aliandaliwa karamu.
Wengi walimsifu kama mwana wa kike aliye na heshima zake.
Wazazi walimletea zawadi binti huyu kama shukrani zao za dhati.
Walimu walinena mengi ya mibaraka kwake mwalimu mwenza mtarajiwa.
Wanafunzi walitunga sifo. Yaliyonenwa na kufanywa ile siku kuu ya shukrani zake yangetosha kuandika hiki kitabu. Yangezidi filamu taajika ulimwenguni na magezetini haya yangepata wasomaji wengi.
Hakika huyu mwana wa kike alikuwa moto usiochoma. Alinata mioyo ya wengi popote alipopita kama Pendo.
Jioni ile baada ya sherehe,Pendo alingoa nanga hadi mjini ile aendelee na masomo yake katika chuo kikuu cha Nairobi.
***
Usiku ule Rashid walipopata chakula cha jioni,aliota njozi ya kutosahaulika maishani mwake.
Alikiuwa mfalme aliyemiliki himaya ya Nairobi. Alijihisi mwenye nguvu hasa alipokuwa mbavuni mwa malkia wake Pendo.
Popote alipoenda alikuwa na huyu sabuni wake  wa mishipa na hewa yake kwa wake.
Wakati mmoja walipokuwa wanatoka kusali kanisani,alikuta walinzi wake wameacha lango wazi.
Lango lenyewe halikuwa wazi kiasi cha mwivi kuona ila ni kusahau komeo. Upepo ulipokuwa unapuliza kulikuwa na mwanya wa tundu la shindano aliloliona alipopiga honi pale.
“Hawa walinzi hau walinda nzi”aliongea kwa hamaki.
Alirusharusha fimbo yake juu juu alivyozoea wakati wa hamaki.
“Wanastahili kupigwa karamu na kuajiri wanatoka kulinda kazi,”
“Sivyo mpenzi wangu,kumbuka tumetoka kanisani,” Pendo alisema huku akimpapasa mumewe begani.
Rashid alihema kiasi na kumtazama malkia wake machoni.
“Mume wangu usiwe na hasira kiasi hicho,pasta alisema tusiwe wenye hasira…”
“Sawa mke wangu ila…”
“Sio ila tena,tuliza moyo,tuingie kwa gari kabla ya wapita njia na wanahabari kupata ya magazetini,” mkewe alimshawishi mfalme.
Rashid alikubali huku wote wakitabasamu wakielekea ndani ya gari.
Walikuwa na msafara wa magari ya kifahari. Wao walikuwa kwa Passat.Mbele kulikuwa na magari aina ya prado, benz na subaru . Waliongozwa nyuma na Land Rover,Subaru…
Ndoto yake ilikatizwa na kilio cha mtoto,mmoja wa wapangaji.
                                                      ***

Thursday, September 1, 2016

SURA YA 4
Pendo alitazama simu ikikiriza hadi ikakoma. Ilipigwa tena mara ya pili hakuchukua.
Alipoona imepigwa mara ya tatu alimua kuchukua hatua ya kuzungumza na kujua nia ya mpigaji.
“mambo vipi Pendo,”
“niko mzima nashukuru. Nani mwezengu?
“haah!hauwezi tambua sauti?”
“mmmh!”
“jina langu ni Rashid,ulinisaidia miezi sita iliyopita pale Tom Mboya Street usiku,”
“Ohoo!muda mrefu sana,naamini huu salama na uko mjini bado?”
“Ndio nimo humu humu,mji wa jua vile wanavyosema wakweli kama si utani.”
“Una umachachari sana. Nani kakupa nambari za kwangu za simu.”
“hizo ni habari za siku nyingine. Nimekupigia simu kwanza nikusalimu na mwisho pokea shukrani zangu kwa ule usaidizi wako kwangu.nashukuru sana.”
“Karibu kaka.”
Pendo aliendelea na mchezo wake wa simu baada ya kuzungumza naye Rashid.
Muda ulizidi kupiga hatua na jioni kukaribia. Ilimbidi Pendo ajiandae kwenda sokoni kununua vya jikoni. Popote alipokuwa alikuwa pekee yake. Alikuwa na hulka ya ‘ubnafsi’ yaani hakupenda maneno mengi. Kamwe alijua wengi wangemdadisi na pili wapangaji wenza hasa wanawake wanapenda umbea.
***
Alipomwelekeza nduguye bafu ilipo,alirudi akachukua jiko lile lake na miaka sita la chuma na kutayarisha. Aliweka makaa juu, akatoa gazeti kuukuu na akawekelea kwa makaa. Akamimina mafuta taa kiasi. Akawasha kiberiti na kuwekelea juu ya yale magazeti mekoni.
Alitazama moto ule,akajaribu kukagua ule moshi. Alipokazia macho zaidi kwa jiko,alipata jicho lake likitoa machozi. Ule moshi ulikuwa mkali kwake.
Alileta kipepeta na kupepeta ule moto. Miale ya moto iliskika ikifyatua.
Alipohakikisha moshi hapo tena,alichuka jiko yake ndani ya nyubamba.
Alianza kupika ugali kwanza. Alipokuwa anasonga ugali,Barasa alingia kutoka bafuni.
“kaka huku kuna baridi sana”
“ ndio lakini usniambia haukuoga”
Wote walingua kicheko na ilikuwa majira ya saa sita usiku sasa.
“la kaka hata si hivyo nimepotea unajua hizi  nyumba ni mingi sana,”
Barasa alicheka hadi ule ugali ukaungua.
Rashid alishangaa vile nduguye anacheka. Hakuona cha kuchekesha.
Ilikuwa saa nane usiku walipokuwa wanapata chajio.
Rashid alimpa ushuuda Barasa kuhusu matukio ya saa za mti kati pale kituo kikubwa cha mabasi cha Nairobi.
Kilichomwacha kinywa wazi Barasa ni vile nduguye alikutana na Pendo.
Ni nadra watu kama hao kupatikana katika mji mkuu uliozingirwa na wajanja;kuanzia mdogo hadi mkubwa.
“kuwa makini sana mji huu.hapa napokaa wajanja ni wengi kushida wale waliokukaribisha mjini leo. Hakikisha uwendapo napajua nawe elewa unayekaa naye kila sekunde. Hakikisha unakaa kiume na utembee na kitambulisho chako usije ukala kwa polisi.”

“nimekuskia ndugu.”