SURA YA 4
Pendo alitazama simu ikikiriza hadi ikakoma. Ilipigwa tena
mara ya pili hakuchukua.
Alipoona imepigwa mara ya tatu alimua kuchukua hatua ya
kuzungumza na kujua nia ya mpigaji.
“mambo vipi Pendo,”
“niko mzima nashukuru. Nani mwezengu?
“haah!hauwezi tambua sauti?”
“mmmh!”
“jina langu ni Rashid,ulinisaidia miezi sita iliyopita pale Tom Mboya Street usiku,”
“Ohoo!muda mrefu sana,naamini huu salama na uko mjini bado?”
“Ndio nimo humu humu,mji wa jua vile wanavyosema wakweli kama
si utani.”
“Una umachachari sana. Nani kakupa nambari za kwangu za simu.”
“hizo ni habari za siku nyingine. Nimekupigia simu kwanza
nikusalimu na mwisho pokea shukrani zangu kwa ule usaidizi wako
kwangu.nashukuru sana.”
“Karibu kaka.”
Pendo aliendelea na mchezo wake wa simu baada ya kuzungumza
naye Rashid.
Muda ulizidi kupiga hatua na jioni kukaribia. Ilimbidi Pendo
ajiandae kwenda sokoni kununua vya jikoni. Popote alipokuwa alikuwa pekee yake.
Alikuwa na hulka ya ‘ubnafsi’ yaani hakupenda maneno mengi. Kamwe alijua wengi
wangemdadisi na pili wapangaji wenza hasa wanawake wanapenda umbea.
***
Alipomwelekeza nduguye bafu ilipo,alirudi akachukua jiko lile
lake na miaka sita la chuma na kutayarisha. Aliweka makaa juu, akatoa gazeti
kuukuu na akawekelea kwa makaa. Akamimina mafuta taa kiasi. Akawasha kiberiti
na kuwekelea juu ya yale magazeti mekoni.
Alitazama moto ule,akajaribu kukagua ule moshi. Alipokazia macho
zaidi kwa jiko,alipata jicho lake likitoa machozi. Ule moshi ulikuwa mkali
kwake.
Alileta kipepeta na kupepeta ule moto. Miale ya moto iliskika
ikifyatua.
Alipohakikisha moshi hapo tena,alichuka jiko yake ndani ya
nyubamba.
Alianza kupika ugali kwanza. Alipokuwa anasonga ugali,Barasa
alingia kutoka bafuni.
“kaka huku kuna baridi sana”
“ ndio lakini usniambia haukuoga”
Wote walingua kicheko na ilikuwa majira ya saa sita usiku
sasa.
“la kaka hata si hivyo nimepotea unajua hizi nyumba ni mingi sana,”
Barasa alicheka hadi ule ugali ukaungua.
Rashid alishangaa vile nduguye anacheka. Hakuona cha
kuchekesha.
Ilikuwa saa nane usiku walipokuwa wanapata chajio.
Rashid alimpa ushuuda Barasa kuhusu matukio ya saa za mti kati
pale kituo kikubwa cha mabasi cha Nairobi.
Kilichomwacha kinywa wazi Barasa ni vile nduguye alikutana na
Pendo.
Ni nadra watu kama hao kupatikana katika mji mkuu
uliozingirwa na wajanja;kuanzia mdogo hadi mkubwa.
“kuwa makini sana mji huu.hapa napokaa wajanja ni wengi
kushida wale waliokukaribisha mjini leo. Hakikisha uwendapo napajua nawe elewa
unayekaa naye kila sekunde. Hakikisha unakaa kiume na utembee na kitambulisho
chako usije ukala kwa polisi.”
“nimekuskia ndugu.”
No comments:
Post a Comment