SURA YA 3
Pendo aligutushwa kutoka lindi la mawazo na harufu ya maziwa.
Aliasahau kuwa alikuwa ameweka maziwa kwenye gesi ya chai ya saa kumi.
Aliamuka mbio hadi jikoni na kuzima ile gesi.
Alibadilisha yale maziwa kwenda ndani ya sufuria nyingine. Baadaye
aliwasha moto tena na sasa kuweka fikira zake jikoni.
Kuolewa ni sheria,
Kuzaa ni majaliwa
Ndoa kuifurahia ni mtoto kuzaliwa…
Aliimba wimbo wake huu Nyota Ndogo huku akiweka sukari kwenye
kichungi na kutia majani ya tangawizi ndani ya maziwa.
Akaongeza sukari,akakoroga koroga kisha akaiwacha ikatokota.
Alichunga ile chai kwenye jagi
.Halafu akaipeleka mezani baada ya kujitayarishia kikombe kimoja
kilichokalia kisahani cha kijuma hivi kilimgonja pale mezani.
Pendo alienda kochini kuketi huku miguu imechora nne
sebuleni.
Alikunywa ile chai bila haraka huku akibonyeza rununu yake.
“huu mchezo wa Tempo
Run ni mzuri.”
Aliambia nafsi yake.
Alipokuwa anaedelea na shughuli zake za chai na simu,simu
ilikiriza. Nambari hiyo hakumfahamu mwenyewe.
‘nani huyu asiye na taarifa kuwa nina shughuli na Tempo Run?’alijiuliza moyoni.
***
Baraza alifika pale walipokuwa punde tu alipopigiwa simu.
“hujamboo dada”
“sijamboo”
“we bwana mdogo mbona nguo zako zimechanika hivi au umekuja
kwa mguu kutoka nyumbani hadi Nairobi?”
“ni hadithi ndefu ndugu”
Baraza alijuana na Pendo na pia alimshukuru kwa wema wake.
Waliagana usiku ule.
Baraza na nduguye Rashid waliandamana sako kwa bako hadi
kituo cha magari pale Bus Station .Waliabiri
gari huku sasa wakipiga gumzi.
“nyumbani watu wazima?”
“wote wazima walituma salamu,”
“asante.”
“Pesa hapo nyuma oyaa,” utingo alisema.
Kisha Barasa akatoa noti ya shilling mia tano na kumpa.
“una chapa ndogo bosi,sina baki ya hii noti,”
Baraza alikumbuka alikuwa na noti ya shilling ishirini na ile
iliyokuwa mfuko wa wa ndani wa koti lake ya shilingi tano.
Alitoa akampa yule konda
vile alivyojulikana.
“Safi ndugu ila usinijaribu na manoti makubwa makubwa kama
hayo,”
Mawasiliano ya Baraza na Rashid yalikatizwa alipokuwa analipa
nauli.
Dirishani Rashid aliona taa zikiwaka nje na dunia kuzunguka,watu
bado wanatembea na wachuuzi wakiwa kazini kama kawaida yao.
Alifananishi mianga ile kama mji wa Zayuni unaometa meta vile ilivyo katika biblia takatifu .
Walishukia Eastleigh Section 2 tena wakachukua piki piki au boda boda usiku ule.
Walipenye kwenye vichorochoro huku mwendeshaji boda boda
akitumia tajriba yake kuhepa mitaro,mawe bila kuangusha abiria wake.
Nyumba zilikuwa za mabati. Zilikuwa na umeme. Zaidi ya hapo
zote zilifanana.
Njiani watu walikuwa walizidi kupungua.
Baraza alisema “hapo mbele kwa matuta,”
“sawa,” mwendeshaji alimjibu.
Huku nyuma vile walikuwa wamepanda wawili,Rashidi alikuwa
anatoa jasho mikononi kwa kushikilia kile kichuma.
Baraza alimlipa ndururu mbili.
Kiguu na njia wakafika alipokuwa anaiishi Baraza. Ulikuwa mlango
nambari 72 na uliandikwa kwa makaa.
“karibu ndugu”
“Asante”
Aliwasha stima na kumnyesha akati pale kitandani.
Alimwekea maji kwa besheni na kumwonyesha maliwatoni.
Akampa pia na nguo za kubadilisha.
***