SURA YA KWANZA
Pendo alikuwa binti ambaye aila yake hakuna aliyeifahamu
vizuri. Kwa wanaume huyu alikuwa moto wa kuotea mbali. Si eti alikuwa na ukali
wa simba wala kupenda chochote kama mafisi.
Alikuwa mrembo zaidi ya jina lenyewe. Kwa wanawake pale Ghorofani Estate alikuwa
tishio kubwa. Wenyewe walisema kimya kimya,”iweje binti mrembo kiasi hii hana
familia?” “inawezekana ana virusi vya
ukimwi (VVU vile walivyoita).”Kwa watoto huyu alikuwa mfano bora. Alikuwa mwana
wa kike mwenye bidii ya mchwa. Kazi za nyumbani alikuwa gwiji. Shuleni alikuwa mwalimu
shujaa.Kwa mawasiliano alikuwa na adabu.
Yaani ni mtu wa uhusiano mwema na watu.
Popote Pendo alipokuwa, alikuwa pekee yake. Gengeni,shuleni,nyumbani
alikuwa Pendo tu. Katika chuo kikuu alikuwa mwanamtindo aliyejiheshimu kuliko
wote. Mavazi yalimfaa. Ngozi ya kizungu alibarikiwa
nayo. Nywele ndefu kama za wahabeshi alimiliki. Macho ya usingizi na sauti ya ninga yote
yake. Pua refu na laini anayo.Kinywa kinachometameta metu metu bado ni Pendo
huyo.Mashavu yaliyonyooka,shingo,kivua,tumbo…yote ni baadhi ya baraka anazo. Hakika
Muumba alimuumba kabla hajachoka.
Duniani usiogope,wala ukope,
Usipende w’kupe,hata kope,
Pendo usimpe,tena usikope,
Wazazi walipaa,nikabaki paa.
Pendo alijitungia hili shairi na kulitundika ukutani. Aliambatanisha
na picha yake. Picha ya tabasamu la pendo.
***
Pendo alienda shule ya upili ya Gizani kama mwalimu. Alikuwa katika
masomo yake ya nyanjani. Alifundisha somo la Historia na Kemia. Wanafunzi
walimpenda sana kipindi kile alikuwa pale. Somo lake wanafunzi walipita sana. Ungedhani
aliwanywesha maji yakukata kiu cha Kemia na Historia. Shule ya Gizani
ilitunukiwa zawadi katika masomo hayo.
Mbali na kufunza pia aliwaonyesha wanafunzi njia ya kujikimu
kimaisha. Aliazisha kundi la vijana linaloshughulikia kilimo biashara. Wasichana
walijua jinsi ya kusonga nywele na kutumia mashine za kinyozi za kisasa. Kwa walimu aliwazishia chama.shuleni hakuwa vitabu na mitihani tu,hata pesa zilikuwa. Akawa
mfano bora kwa wakubwa na wadogo.
Mengi aliyafanya kwa muda mfupi ungedhani alifanya miaka kumi
iliyopita. Katika tamasha Shule ya upili ya Gizani ilingaa hadi kimataifa.
Pendo anakumbuka ayami moja katika tamasha la wilaya. Jua halikua
kali na baridi ilikuwa na heshima Jumatano ile.
“Tuzo hili si langu. Si la kundi letu la Gizani. Si la mtu
yeyote hivi hivi…” Mrefu mmoja wa wanafunzi wa Gizani alikuwa akitoa hotuba
baada ya kutunikiwa zawadi. Zawadi ya kundi bora katika tamasha za nyimbo za
kitamaduni.
Mrefu alivuta pumzi alipokuwa akiendelea kunena mbele ya
hadhira. Waziri wa michezo na tamadani alikuwa pale ukumbini. Watu walitulia
tuli. Walingoja neno lingine kutoka kinywa cha mnenaji. Kimya kilistiri mle
ndani.
“…tuzo hili ni zawadi pekee, ni shukrani za dhati, ni baraka ya
kwaheri na nia ya nembo ya pendo letu naye. Ni mtu aliye moto kwetu. Si moto wa
kuchoma. Yeye ni moto usiochoma mwili lakini miale yake ni dawa kwa moyo na
bongo zetu. Si mwingine bali ni…”
No comments:
Post a Comment