Sunday, August 28, 2016

SURA YA PILI
Rashid alikuwa anatoka vijijini.alisafiri na basi la kwanza la nyayo bus kutoka jimbo la Kakamega. Alikuwa na mizigo mingi. Si mahindi si kuku. Si miwa si mihogo. Si nanasi si maembe. Mizio mingine kwenye kikabu na mingine katika gunia,boksi na mingine mkononi. Ilikuwa ni saa sita mchana. Jua lilikuwa katika kituo cha mabasi cha country bus. Alikuwa mgeni pale Nairobi. Aliangaza macho juu chini,mbele nyuma…jasho chembamba kilikuwa kinamtririka. Watu walikuwa wengi na wenye shughuli.
“jambo bosi unaenda kariobangi au jogoo road nikupeleke na troli hadi steji ya magari?” jamaa mmoja alimuuliza.
Rashid alikumbuka kuwa nduguye Barasa alimweleza mjini usimwongeleshe usiyemjua. Mji huo una wenyewe.
Alimpima jamaa huo kutoka kichwani hadi utosini. Alikuwa mwenye miramba mine. Alikuwa mweusi tititi. Urefu wake futi sita. Alivalia suruali zilizozombana. Macho makubwa. Mweusi. Kinywa kinene…
“Kijana vipi wewe bubu?”
“mmh mmh”
“kumbe unaongea na unaniharibia time hapa,utanilipa au sio…”
Kwake Rashid ikawa ni ndoto ya mchana. Hakuamini yale maskio yake yaliskia.
Ghafla bin vuu alishtuka kuona mtu shikilia ile boksi yake. Jogoo alikuwa ndani na kwekwe .
Baadaye vijana wenye troli wakamsingira.bila soni wale wenye troli wakashika kilichowapendeza. Wengine walianza kula miwa,mihogo. La kustajambisha mwingine alikuja na kisu kwa ajili ya kuamkate yule kuku ili awe kitoweo.
“ni mwoga huyu” mmoja alisema kichini chini.
“ni mgeni”
“hajui kuongea”
“anajifanya leo ataonyeshwa wajanja kumliko”
Haya ni baadhi ya maneno yaliyosemewa  Rashid. Yalipitia sikio la kulia na mengine yakiingilia sikio la kushoto.
Alivutwa vutwa kama asiye na kilo. Walimzunguka Rashid na kuanza kumpigia ramli. Walikuwa wakitoa maoni wamfanyie nini na atakayeongoza ni nani.
Wapita njia hawakuwa na haja ya kujua yaliyokuwa yakiendelea pale.
Hakuna aliyemfahamu Rashid.
Jua lilikua linaaga mji na jioni kukaribia.
Rashid aliporwa kila kitu alichokuwa nacho. Alihisi anachomeka moyoni. Alitamani mbingu ipasuke na kumumeza. Yote yakawa bure bilashi. Saa tatu usiku alijipata katika mkabala wa Tom Mboya street na Moi avenue.
Ilikuwa saa tatu na nusu usiku.
Nguo zake zilikuwa vumbi tupu.
Macho yalikuwa mekendu kutokana na kwi kwi kwi zile za mchana.
Ilimbidi kuuliza kila mtu iwapo anamfahamu Baraza nduguye.
Alikuwa anaiishi Kiambiu nyuma ya Eastleigh. Kila aliyeulizwa alikana kwa kutingisha kichwa. Wengine alipowasimamisha walimkondolea macho wakidhani ni chokora pipa.
Wachache kama kina dada alipowauliza walitoroka kabla hajamaliza sentensi.
Mwendo wa saa nne usiku,Rashid alikutana na dada mmoja. Dada huyu alionekana nadhifu na mwenye heshima zake.
Rashid alipomkaribia alimsalimu kwa umbali.
“samahani dada”
“sema niskie bwana mkubwa”
“nauliza kama unamjua Barasa”
“anaishi wapi”
“Eastleigh mtaa wa Kiambiu”
“Una nambari zake za simu?”
“ndiyo ninazo”
Yule binti alitoa kitu mkobani. Kilikuwa kikubwa. Kilijaa mkononi mwake .Kilikuwa na mwanga wa samawati hivi. Kilikuwa na picha yake kwenye kioo. Alianza kubonyeza kile kioo na herufu zilikuwa zikionyesha za alfabeti na za nambari.
“kweli huu mji ni wa wajanja. Iweje mtu ana guza tu kioo kisha maandishi, picha na nambari kuonekana?” alijiuliza kimoyo moyo.
“Hello Barasa”
“Unamajua Rashid”
Niko naye hapa Tom Mboya Stature.
INAENDELEA

***


No comments:

Post a Comment