Wednesday, September 21, 2016

SURA YA TANO
Usiku ule Pendo alipomkuta Rashid alikuwa ametoka masomo yake ya nyanjani pale Gizani skuli.
Alikuwa akibarizi mji mkuu. Kupata hewa ya wajanja. Alikuwa akitoka kupata chajio pale Afya Centre.
Pia alipitia Ken Chic kununua kaukau .alipenda sana kutavuna kaukau alipokuwa mjini.
“ah!sijapitia Taveta Court kuona mavazi mapya.” Alijiambia.
Alielekea pale kuona mavazi hasa ya kujikinga na baridi. Ulikuwa mwezi wa agosti. Huu mwezi kuna baridi na umade sana mjini. Alijipima koti lilojulikana kama trench coat.
Katika harakati za kurudi bwenini kabla ya mlinzi kufunga ndipo alipokutana naye Rashid.
Alimwonea huruma. Hajawai kuwa na moyo wa msamaria mwema kwa mtu yeyote hivo isipokuwa huyu kijana.
Alihisi moyoni kuwa amtendee wema adinasi huyu.
Alipomdadisi moyoni alimwona huyu katu si mjanja wa mjini.
***
Siku ile Pendo alimaliza masomo yake ya nyanjani pale skuli ya Gizani aliandaliwa karamu.
Wengi walimsifu kama mwana wa kike aliye na heshima zake.
Wazazi walimletea zawadi binti huyu kama shukrani zao za dhati.
Walimu walinena mengi ya mibaraka kwake mwalimu mwenza mtarajiwa.
Wanafunzi walitunga sifo. Yaliyonenwa na kufanywa ile siku kuu ya shukrani zake yangetosha kuandika hiki kitabu. Yangezidi filamu taajika ulimwenguni na magezetini haya yangepata wasomaji wengi.
Hakika huyu mwana wa kike alikuwa moto usiochoma. Alinata mioyo ya wengi popote alipopita kama Pendo.
Jioni ile baada ya sherehe,Pendo alingoa nanga hadi mjini ile aendelee na masomo yake katika chuo kikuu cha Nairobi.
***
Usiku ule Rashid walipopata chakula cha jioni,aliota njozi ya kutosahaulika maishani mwake.
Alikiuwa mfalme aliyemiliki himaya ya Nairobi. Alijihisi mwenye nguvu hasa alipokuwa mbavuni mwa malkia wake Pendo.
Popote alipoenda alikuwa na huyu sabuni wake  wa mishipa na hewa yake kwa wake.
Wakati mmoja walipokuwa wanatoka kusali kanisani,alikuta walinzi wake wameacha lango wazi.
Lango lenyewe halikuwa wazi kiasi cha mwivi kuona ila ni kusahau komeo. Upepo ulipokuwa unapuliza kulikuwa na mwanya wa tundu la shindano aliloliona alipopiga honi pale.
“Hawa walinzi hau walinda nzi”aliongea kwa hamaki.
Alirusharusha fimbo yake juu juu alivyozoea wakati wa hamaki.
“Wanastahili kupigwa karamu na kuajiri wanatoka kulinda kazi,”
“Sivyo mpenzi wangu,kumbuka tumetoka kanisani,” Pendo alisema huku akimpapasa mumewe begani.
Rashid alihema kiasi na kumtazama malkia wake machoni.
“Mume wangu usiwe na hasira kiasi hicho,pasta alisema tusiwe wenye hasira…”
“Sawa mke wangu ila…”
“Sio ila tena,tuliza moyo,tuingie kwa gari kabla ya wapita njia na wanahabari kupata ya magazetini,” mkewe alimshawishi mfalme.
Rashid alikubali huku wote wakitabasamu wakielekea ndani ya gari.
Walikuwa na msafara wa magari ya kifahari. Wao walikuwa kwa Passat.Mbele kulikuwa na magari aina ya prado, benz na subaru . Waliongozwa nyuma na Land Rover,Subaru…
Ndoto yake ilikatizwa na kilio cha mtoto,mmoja wa wapangaji.
                                                      ***

Thursday, September 1, 2016

SURA YA 4
Pendo alitazama simu ikikiriza hadi ikakoma. Ilipigwa tena mara ya pili hakuchukua.
Alipoona imepigwa mara ya tatu alimua kuchukua hatua ya kuzungumza na kujua nia ya mpigaji.
“mambo vipi Pendo,”
“niko mzima nashukuru. Nani mwezengu?
“haah!hauwezi tambua sauti?”
“mmmh!”
“jina langu ni Rashid,ulinisaidia miezi sita iliyopita pale Tom Mboya Street usiku,”
“Ohoo!muda mrefu sana,naamini huu salama na uko mjini bado?”
“Ndio nimo humu humu,mji wa jua vile wanavyosema wakweli kama si utani.”
“Una umachachari sana. Nani kakupa nambari za kwangu za simu.”
“hizo ni habari za siku nyingine. Nimekupigia simu kwanza nikusalimu na mwisho pokea shukrani zangu kwa ule usaidizi wako kwangu.nashukuru sana.”
“Karibu kaka.”
Pendo aliendelea na mchezo wake wa simu baada ya kuzungumza naye Rashid.
Muda ulizidi kupiga hatua na jioni kukaribia. Ilimbidi Pendo ajiandae kwenda sokoni kununua vya jikoni. Popote alipokuwa alikuwa pekee yake. Alikuwa na hulka ya ‘ubnafsi’ yaani hakupenda maneno mengi. Kamwe alijua wengi wangemdadisi na pili wapangaji wenza hasa wanawake wanapenda umbea.
***
Alipomwelekeza nduguye bafu ilipo,alirudi akachukua jiko lile lake na miaka sita la chuma na kutayarisha. Aliweka makaa juu, akatoa gazeti kuukuu na akawekelea kwa makaa. Akamimina mafuta taa kiasi. Akawasha kiberiti na kuwekelea juu ya yale magazeti mekoni.
Alitazama moto ule,akajaribu kukagua ule moshi. Alipokazia macho zaidi kwa jiko,alipata jicho lake likitoa machozi. Ule moshi ulikuwa mkali kwake.
Alileta kipepeta na kupepeta ule moto. Miale ya moto iliskika ikifyatua.
Alipohakikisha moshi hapo tena,alichuka jiko yake ndani ya nyubamba.
Alianza kupika ugali kwanza. Alipokuwa anasonga ugali,Barasa alingia kutoka bafuni.
“kaka huku kuna baridi sana”
“ ndio lakini usniambia haukuoga”
Wote walingua kicheko na ilikuwa majira ya saa sita usiku sasa.
“la kaka hata si hivyo nimepotea unajua hizi  nyumba ni mingi sana,”
Barasa alicheka hadi ule ugali ukaungua.
Rashid alishangaa vile nduguye anacheka. Hakuona cha kuchekesha.
Ilikuwa saa nane usiku walipokuwa wanapata chajio.
Rashid alimpa ushuuda Barasa kuhusu matukio ya saa za mti kati pale kituo kikubwa cha mabasi cha Nairobi.
Kilichomwacha kinywa wazi Barasa ni vile nduguye alikutana na Pendo.
Ni nadra watu kama hao kupatikana katika mji mkuu uliozingirwa na wajanja;kuanzia mdogo hadi mkubwa.
“kuwa makini sana mji huu.hapa napokaa wajanja ni wengi kushida wale waliokukaribisha mjini leo. Hakikisha uwendapo napajua nawe elewa unayekaa naye kila sekunde. Hakikisha unakaa kiume na utembee na kitambulisho chako usije ukala kwa polisi.”

“nimekuskia ndugu.”

Tuesday, August 30, 2016

SURA YA 3
Pendo aligutushwa kutoka lindi la mawazo na harufu ya maziwa. Aliasahau kuwa alikuwa ameweka maziwa kwenye gesi ya chai ya saa kumi.
Aliamuka mbio hadi jikoni na kuzima ile gesi.
Alibadilisha yale maziwa kwenda ndani ya sufuria nyingine. Baadaye aliwasha moto tena na sasa kuweka fikira zake jikoni.
Kuolewa ni sheria,
Kuzaa ni majaliwa
Ndoa kuifurahia ni mtoto kuzaliwa…
Aliimba wimbo wake huu Nyota Ndogo huku akiweka sukari kwenye kichungi na kutia majani ya tangawizi ndani ya maziwa.
Akaongeza sukari,akakoroga koroga kisha akaiwacha ikatokota.
Alichunga ile chai kwenye jagi .Halafu akaipeleka mezani baada ya kujitayarishia kikombe kimoja kilichokalia kisahani cha kijuma hivi kilimgonja pale mezani.
Pendo alienda kochini kuketi huku miguu imechora nne sebuleni.
Alikunywa ile chai bila haraka huku akibonyeza rununu yake.
“huu mchezo wa Tempo Run ni mzuri.”
Aliambia nafsi yake.
Alipokuwa anaedelea na shughuli zake za chai na simu,simu ilikiriza. Nambari hiyo hakumfahamu mwenyewe.
‘nani huyu asiye na taarifa kuwa nina shughuli na Tempo Run?’alijiuliza moyoni.
***
Baraza alifika pale walipokuwa punde tu alipopigiwa simu.
“hujamboo dada”
“sijamboo”
“we bwana mdogo mbona nguo zako zimechanika hivi au umekuja kwa mguu kutoka nyumbani hadi Nairobi?”
“ni hadithi ndefu ndugu”
Baraza alijuana na Pendo na pia alimshukuru kwa wema wake.
Waliagana usiku ule.
Baraza na nduguye Rashid waliandamana sako kwa bako hadi kituo cha magari pale Bus Station .Waliabiri gari huku sasa wakipiga gumzi.
“nyumbani watu wazima?”
“wote wazima walituma salamu,”
“asante.”
“Pesa hapo nyuma oyaa,” utingo alisema.
Kisha Barasa akatoa noti ya shilling mia tano na kumpa.
“una chapa ndogo bosi,sina baki ya hii noti,”
Baraza alikumbuka alikuwa na noti ya shilling ishirini na ile iliyokuwa mfuko wa wa ndani wa koti lake ya shilingi tano.
Alitoa akampa yule konda vile alivyojulikana.
“Safi ndugu ila usinijaribu na manoti makubwa makubwa kama hayo,”
Mawasiliano ya Baraza na Rashid yalikatizwa alipokuwa analipa nauli.
Dirishani Rashid aliona taa zikiwaka nje na dunia kuzunguka,watu bado wanatembea na wachuuzi wakiwa kazini kama kawaida yao.
Alifananishi mianga ile kama mji wa Zayuni unaometa meta vile ilivyo katika biblia takatifu .
Walishukia Eastleigh Section 2 tena wakachukua piki piki au boda boda usiku ule.
Walipenye kwenye vichorochoro huku mwendeshaji boda boda akitumia tajriba yake kuhepa mitaro,mawe bila kuangusha abiria wake.
Nyumba zilikuwa za mabati. Zilikuwa na umeme. Zaidi ya hapo zote zilifanana.
Njiani watu walikuwa walizidi kupungua.
Baraza alisema “hapo mbele kwa matuta,”
“sawa,” mwendeshaji alimjibu.
Huku nyuma vile walikuwa wamepanda wawili,Rashidi alikuwa anatoa jasho mikononi kwa kushikilia kile kichuma.
Baraza alimlipa ndururu mbili.
Kiguu na njia wakafika alipokuwa anaiishi Baraza. Ulikuwa mlango nambari 72 na uliandikwa kwa makaa.
“karibu ndugu”
“Asante”
Aliwasha stima na kumnyesha akati pale kitandani.
Alimwekea maji kwa besheni na kumwonyesha maliwatoni.
Akampa pia na nguo za kubadilisha.
***



Sunday, August 28, 2016

SURA YA PILI
Rashid alikuwa anatoka vijijini.alisafiri na basi la kwanza la nyayo bus kutoka jimbo la Kakamega. Alikuwa na mizigo mingi. Si mahindi si kuku. Si miwa si mihogo. Si nanasi si maembe. Mizio mingine kwenye kikabu na mingine katika gunia,boksi na mingine mkononi. Ilikuwa ni saa sita mchana. Jua lilikuwa katika kituo cha mabasi cha country bus. Alikuwa mgeni pale Nairobi. Aliangaza macho juu chini,mbele nyuma…jasho chembamba kilikuwa kinamtririka. Watu walikuwa wengi na wenye shughuli.
“jambo bosi unaenda kariobangi au jogoo road nikupeleke na troli hadi steji ya magari?” jamaa mmoja alimuuliza.
Rashid alikumbuka kuwa nduguye Barasa alimweleza mjini usimwongeleshe usiyemjua. Mji huo una wenyewe.
Alimpima jamaa huo kutoka kichwani hadi utosini. Alikuwa mwenye miramba mine. Alikuwa mweusi tititi. Urefu wake futi sita. Alivalia suruali zilizozombana. Macho makubwa. Mweusi. Kinywa kinene…
“Kijana vipi wewe bubu?”
“mmh mmh”
“kumbe unaongea na unaniharibia time hapa,utanilipa au sio…”
Kwake Rashid ikawa ni ndoto ya mchana. Hakuamini yale maskio yake yaliskia.
Ghafla bin vuu alishtuka kuona mtu shikilia ile boksi yake. Jogoo alikuwa ndani na kwekwe .
Baadaye vijana wenye troli wakamsingira.bila soni wale wenye troli wakashika kilichowapendeza. Wengine walianza kula miwa,mihogo. La kustajambisha mwingine alikuja na kisu kwa ajili ya kuamkate yule kuku ili awe kitoweo.
“ni mwoga huyu” mmoja alisema kichini chini.
“ni mgeni”
“hajui kuongea”
“anajifanya leo ataonyeshwa wajanja kumliko”
Haya ni baadhi ya maneno yaliyosemewa  Rashid. Yalipitia sikio la kulia na mengine yakiingilia sikio la kushoto.
Alivutwa vutwa kama asiye na kilo. Walimzunguka Rashid na kuanza kumpigia ramli. Walikuwa wakitoa maoni wamfanyie nini na atakayeongoza ni nani.
Wapita njia hawakuwa na haja ya kujua yaliyokuwa yakiendelea pale.
Hakuna aliyemfahamu Rashid.
Jua lilikua linaaga mji na jioni kukaribia.
Rashid aliporwa kila kitu alichokuwa nacho. Alihisi anachomeka moyoni. Alitamani mbingu ipasuke na kumumeza. Yote yakawa bure bilashi. Saa tatu usiku alijipata katika mkabala wa Tom Mboya street na Moi avenue.
Ilikuwa saa tatu na nusu usiku.
Nguo zake zilikuwa vumbi tupu.
Macho yalikuwa mekendu kutokana na kwi kwi kwi zile za mchana.
Ilimbidi kuuliza kila mtu iwapo anamfahamu Baraza nduguye.
Alikuwa anaiishi Kiambiu nyuma ya Eastleigh. Kila aliyeulizwa alikana kwa kutingisha kichwa. Wengine alipowasimamisha walimkondolea macho wakidhani ni chokora pipa.
Wachache kama kina dada alipowauliza walitoroka kabla hajamaliza sentensi.
Mwendo wa saa nne usiku,Rashid alikutana na dada mmoja. Dada huyu alionekana nadhifu na mwenye heshima zake.
Rashid alipomkaribia alimsalimu kwa umbali.
“samahani dada”
“sema niskie bwana mkubwa”
“nauliza kama unamjua Barasa”
“anaishi wapi”
“Eastleigh mtaa wa Kiambiu”
“Una nambari zake za simu?”
“ndiyo ninazo”
Yule binti alitoa kitu mkobani. Kilikuwa kikubwa. Kilijaa mkononi mwake .Kilikuwa na mwanga wa samawati hivi. Kilikuwa na picha yake kwenye kioo. Alianza kubonyeza kile kioo na herufu zilikuwa zikionyesha za alfabeti na za nambari.
“kweli huu mji ni wa wajanja. Iweje mtu ana guza tu kioo kisha maandishi, picha na nambari kuonekana?” alijiuliza kimoyo moyo.
“Hello Barasa”
“Unamajua Rashid”
Niko naye hapa Tom Mboya Stature.
INAENDELEA

***


Friday, August 26, 2016

SURA YA KWANZA
Pendo alikuwa binti ambaye aila yake hakuna aliyeifahamu vizuri. Kwa wanaume huyu alikuwa moto wa kuotea mbali. Si eti alikuwa na ukali wa simba wala kupenda chochote kama mafisi. Alikuwa mrembo zaidi ya jina lenyewe. Kwa wanawake pale Ghorofani Estate alikuwa tishio kubwa. Wenyewe walisema kimya kimya,”iweje binti mrembo kiasi hii hana familia?”  “inawezekana ana virusi vya ukimwi (VVU vile walivyoita).”Kwa watoto huyu alikuwa mfano bora. Alikuwa mwana wa kike mwenye bidii ya mchwa. Kazi za nyumbani alikuwa gwiji. Shuleni alikuwa mwalimu shujaa.Kwa  mawasiliano alikuwa na adabu. Yaani ni mtu wa uhusiano mwema na watu.
Popote Pendo alipokuwa, alikuwa pekee yake. Gengeni,shuleni,nyumbani alikuwa Pendo tu. Katika chuo kikuu alikuwa mwanamtindo aliyejiheshimu kuliko wote. Mavazi yalimfaa. Ngozi ya kizungu alibarikiwa  nayo. Nywele ndefu kama za wahabeshi alimiliki. Macho ya usingizi na sauti ya ninga yote yake. Pua refu na laini anayo.Kinywa kinachometameta metu metu bado ni Pendo huyo.Mashavu yaliyonyooka,shingo,kivua,tumbo…yote ni baadhi ya baraka anazo. Hakika Muumba alimuumba  kabla hajachoka.
Duniani usiogope,wala ukope,
Usipende w’kupe,hata kope,
Pendo usimpe,tena usikope,
Wazazi walipaa,nikabaki paa.
Pendo alijitungia hili shairi na kulitundika ukutani. Aliambatanisha na picha yake. Picha ya tabasamu la pendo.
                                                                         ***
Pendo alienda shule ya upili ya Gizani kama mwalimu. Alikuwa katika masomo yake ya nyanjani. Alifundisha somo la Historia na Kemia. Wanafunzi walimpenda sana kipindi kile alikuwa pale. Somo lake wanafunzi walipita sana. Ungedhani aliwanywesha maji yakukata kiu cha Kemia na Historia. Shule ya Gizani ilitunukiwa zawadi katika masomo hayo.
Mbali na kufunza pia aliwaonyesha wanafunzi njia ya kujikimu kimaisha. Aliazisha kundi la vijana linaloshughulikia kilimo biashara. Wasichana walijua jinsi ya kusonga nywele na kutumia mashine za kinyozi za kisasa. Kwa  walimu aliwazishia chama.shuleni hakuwa vitabu na mitihani tu,hata pesa zilikuwa. Akawa mfano bora kwa wakubwa na wadogo.
Mengi aliyafanya kwa muda mfupi ungedhani alifanya miaka kumi iliyopita. Katika tamasha Shule ya upili ya Gizani ilingaa hadi kimataifa.
Pendo anakumbuka ayami moja katika tamasha la wilaya. Jua halikua kali na baridi ilikuwa na heshima Jumatano ile.
“Tuzo hili si langu. Si la kundi letu la Gizani. Si la mtu yeyote hivi hivi…” Mrefu mmoja wa wanafunzi wa Gizani alikuwa akitoa hotuba baada ya kutunikiwa zawadi. Zawadi ya kundi bora katika tamasha za nyimbo za kitamaduni.
Mrefu alivuta pumzi alipokuwa akiendelea kunena mbele ya hadhira. Waziri wa michezo na tamadani alikuwa pale ukumbini. Watu walitulia tuli. Walingoja neno lingine kutoka kinywa cha mnenaji. Kimya kilistiri mle ndani.

“…tuzo hili ni zawadi pekee, ni shukrani za dhati, ni baraka ya kwaheri na nia ya nembo ya pendo letu naye. Ni mtu aliye moto kwetu. Si moto wa kuchoma. Yeye ni moto usiochoma mwili lakini miale yake ni dawa kwa moyo na bongo zetu. Si mwingine bali ni…”
                                                 
#INAENDELEA

Thursday, August 25, 2016

kazi ipi sasa

                                                                                               Kazi ipi sasa


Asubuhi damka,siku tayarisha,
Kazini nafika,mie najitayarisha,
Shajara naandika,kalamu inaaisha,
Naajiuliza kaka,kazi ipi sasa?

Stima inakatika,moyoni nakatika,
Maji inakatika,kiu kinakatika,
Jokofu imekatika,mawazo yamekatika,
Naajiuliza kaka,kazi ipi sasa?

Kazini nafunga,nifanyalo siafahamu,
Akilini nimefunga,nifikirialo sifahamu,
Mwilini nimeunga,niwazalo sifahamu,
Naajiuliza kaka,kazi ipi sasa?



Hela sina,hesabu haipigiki,
Sioni sana,sipangui sipangiki,
Mimi najikana,najiuma siumiki,
Kaka najiuliza,kazi ipi sasa?

Kuamka tisa saa,jogoo kawika,
Naloa maji saa,uchovu kanitwika,
Miayo natoa saa,kumbe ndotoka,
Ndoto hii saa,kaota usikuka.

                                 NA NYABUTO HENRY